Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hosea 1:6 - Swahili Revised Union Version

6 Akachukua mimba tena, akazaa mtoto wa kike, BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Gomeri alipata mimba tena, akazaa mtoto wa kike. Mwenyezi-Mungu akamwambia Hosea, “Mpe mtoto huyo jina ‘Asiyehurumiwa’, maana sitawahurumia tena Waisraeli wala sitawasamehe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Gomeri alipata mimba tena, akazaa mtoto wa kike. Mwenyezi-Mungu akamwambia Hosea, “Mpe mtoto huyo jina ‘Asiyehurumiwa’, maana sitawahurumia tena Waisraeli wala sitawasamehe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Gomeri alipata mimba tena, akazaa mtoto wa kike. Mwenyezi-Mungu akamwambia Hosea, “Mpe mtoto huyo jina ‘Asiyehurumiwa’, maana sitawahurumia tena Waisraeli wala sitawasamehe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhama, kwa maana sitaonesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. Kisha bwana akamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhama, kwa maana sitaonyesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Akachukua mimba tena, akazaa mtoto wa kike, BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.

Tazama sura Nakili

Hosea 1:6
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi BWANA akakikataa kizazi chote cha Israeli, akawatesa, na kuwatia katika mikono ya watu wenye kuwateka nyara, hata alipokwisha kuwatupa, watoke machoni pake.

Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.

Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.

Basi, akiisha kumwachisha Lo-ruhama kunyonya, akachukua mimba, akazaa mtoto wa kiume.

Nami nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu.

naam, sitawaonea rehema watoto wake; kwa maana ni watoto wa uzinzi.

BWANA akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona timazi. Ndipo Bwana akasema, Tazama, nitaweka timazi kati ya watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe;

Angalieni, macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema BWANA.

ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo