Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu, Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu.
Maombolezo 4:8 - Swahili Revised Union Version Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa; Hawajulikani katika njia kuu; Ngozi yao yagandamana na mifupa yao Imekauka, imekuwa kama mti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa sura zao ni nyeusi kuliko makaa, wanapita barabarani bila kujulikana; ngozi yao imegandamana na mifupa yao imekauka, imekuwa kama kuni. Biblia Habari Njema - BHND Sasa sura zao ni nyeusi kuliko makaa, wanapita barabarani bila kujulikana; ngozi yao imegandamana na mifupa yao imekauka, imekuwa kama kuni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa sura zao ni nyeusi kuliko makaa, wanapita barabarani bila kujulikana; ngozi yao imegandamana na mifupa yao imekauka, imekuwa kama kuni. Neno: Bibilia Takatifu Lakini sasa ni weusi kuliko masizi; hawatambulikani barabarani. Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao, imekuwa mikavu kama fimbo. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini sasa ni weusi kuliko masizi; hawatambulikani barabarani. Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao, imekuwa mikavu kama fimbo. BIBLIA KISWAHILI Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa; Hawajulikani katika njia kuu; Ngozi yao yagandamana na mifupa yao Imekauka, imekuwa kama mti. |
Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu, Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu.
Basi walipoinua macho yao, wakiwa bado kwa mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho lake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni.
Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu.
Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),
Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagonganagongana; moyoni kote mna uchungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.
Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung'uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.