Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Maombolezo 4:7 - Swahili Revised Union Version

7 Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Vijana wa Siyoni walikuwa safi kuliko theluji, walikuwa weupe kuliko maziwa. Miili yao ilikuwa myekundu kama matumbawe, uzuri wa viwiliwili vyao kama johari ya rangi ya samawati.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Vijana wa Siyoni walikuwa safi kuliko theluji, walikuwa weupe kuliko maziwa. Miili yao ilikuwa myekundu kama matumbawe, uzuri wa viwiliwili vyao kama johari ya rangi ya samawati.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Vijana wa Siyoni walikuwa safi kuliko theluji, walikuwa weupe kuliko maziwa. Miili yao ilikuwa myekundu kama matumbawe, uzuri wa viwiliwili vyao kama johari ya rangi ya samawati.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Wakuu wao walikuwa wameng’aa kuliko theluji na weupe kuliko maziwa, miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani, kuonekana kwao kama yakuti samawi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Wakuu wao walikuwa wameng’aa kuliko theluji na weupe kuliko maziwa, miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani, kuonekana kwao kama yakuti samawi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi.

Tazama sura Nakili

Maombolezo 4:7
15 Marejeleo ya Msalaba  

Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi.

Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani.

Wavulana wetu wakiwa ujanani wawe kama miche Iliyostawi kikamilifu. Binti zetu wawe kama nguzo za pembeni Zilizochongwa ili kupamba kasri.

Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake.

Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu, Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi;

Miguu yake ni kama nguzo za marimari, Zilizowekwa juu ya misingi ya dhahabu; Sura yake ni kama Lebanoni, Ni bora mfano wa mierezi;

Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.

Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.

kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.

lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hadi siku ya kufa kwake.

Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.

Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo