Basi, Yeremia alipokuwa ameingia katika nyumba ya shimo, na katika vyumba vya ndani; na Yeremia alipokuwa amekaa humo siku nyingi;
Maombolezo 3:53 - Swahili Revised Union Version Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walinitupa shimoni nikiwa hai na juu yangu wakarundika mawe. Biblia Habari Njema - BHND Walinitupa shimoni nikiwa hai na juu yangu wakarundika mawe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walinitupa shimoni nikiwa hai na juu yangu wakarundika mawe. Neno: Bibilia Takatifu Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo na kunitupia mawe; Neno: Maandiko Matakatifu Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo na kunitupia mawe; BIBLIA KISWAHILI Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu. |
Basi, Yeremia alipokuwa ameingia katika nyumba ya shimo, na katika vyumba vya ndani; na Yeremia alipokuwa amekaa humo siku nyingi;
Na sasa unisikilize, Ee bwana wangu mfalme; maombi yangu yakapate kibali mbele yako; usinirudishe nyumbani mwa Yonathani, mwandishi, nisije nikafa humo.
Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika ukumbi wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo.
Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hakuna mkate kabisa katika mji.
Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia mhuri kwa mhuri wake mwenyewe, na kwa mhuri wa wakuu wake, lisibadilike neno lolote katika habari za Danieli.
Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.
akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe mhuri, pamoja na kuwaweka wale askari walinzi.