Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 6:18 - Swahili Revised Union Version

18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kisha mfalme akarudi katika ikuluni yake ambamo alikesha akifunga; hakufanya tafrija ya aina yoyote, na usingizi ukampaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Kisha mfalme akarudi katika ikuluni yake ambamo alikesha akifunga; hakufanya tafrija ya aina yoyote, na usingizi ukampaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kisha mfalme akarudi katika ikuluni yake ambamo alikesha akifunga; hakufanya tafrija ya aina yoyote, na usingizi ukampaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kisha mfalme akarudi kwenye jumba lake la kifalme, naye usiku kucha hakuweza kula wala kutumia viburudisho alivyoletewa, na hakuweza kulala.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kisha mfalme akarudi kwenye jumba lake la kifalme, naye usiku kucha hakula chakula wala kutumia viburudisho alivyoletewa. Lakini hakuweza kulala.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

18 Kisha mfalme akaenda jumbani mwake, akalala na kufunga mfungo, hata wakeze hakuwaingiza mwake, lakini usingizi hakuupata.

Tazama sura Nakili




Danieli 6:18
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Mefiboshethi, mwana wa Sauli, akashuka ili amlaki mfalme; alikuwa hakukata kucha za miguu yake wala kukata ndevu zake, wala kufua nguo zake, tangu siku alipoondoka mfalme, hadi siku hiyo aliporudi kwake kwa amani.


Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole.


Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha kumbukumbu nacho kikasomwa mbele ya mfalme.


Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi.


Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.


Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Nilitaabika nisiweze kunena.


tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, wanaume kwa wanawake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana.


Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu.


Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia.


Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadneza, Nebukadneza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, akatokwa na usingizi.


Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba.


Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikika ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yoyote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo