Kwa maana nitawezaje kumwendea baba yangu, na huyu kijana hayuko pamoja nami? Nisije nikayaona mabaya yatakayompata baba yangu.
Maombolezo 3:51 - Swahili Revised Union Version Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu, Kwa ajili ya kuangamizwa kwa binti wa watu wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nalia na kujaa majonzi, kuona yaliyowapata kina mama wa mji wangu. Biblia Habari Njema - BHND Nalia na kujaa majonzi, kuona yaliyowapata kina mama wa mji wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nalia na kujaa majonzi, kuona yaliyowapata kina mama wa mji wangu. Neno: Bibilia Takatifu Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu. BIBLIA KISWAHILI Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu, Kwa ajili ya kuangamizwa kwa binti wa watu wangu. |
Kwa maana nitawezaje kumwendea baba yangu, na huyu kijana hayuko pamoja nami? Nisije nikayaona mabaya yatakayompata baba yangu.
Kwa sababu hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaadhibu watu hawa; vijana watakufa kwa upanga; wana wao na binti zao watakufa kwa njaa;
Na watu hao, waliopewa unabii na wao, watatupwa nje katika njia kuu za Yerusalemu kwa sababu ya upanga na njaa; wala hawatakuwa na mtu wa kuwazika, wao na wake zao, na wana wao, na binti zao; maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.
Nikitoka kwenda shambani, tazama, wako huko waliouawa kwa upanga! Na nikiingia mjini, tazama, wamo humo wanaougua kwa sababu ya njaa! Maana nabii na kuhani, wote wawili, huenda huku na huko katika nchi, wala hawana maarifa.
Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.
BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.
Macho yangu yamechoka kwa machozi, Mtima wangu umetaabika; Ini langu linamiminwa juu ya nchi Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu; Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao, Huzimia katika mitaa ya mji.
Kijana na mzee hulala chini Katika njia kuu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wameanguka kwa upanga; Umewaua katika siku ya hasira yako; Umeua, wala hukuona huruma.