Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 1:18 - Swahili Revised Union Version

18 BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 “Lakini Mwenyezi-Mungu amefanya sawa kwa maana nimeliasi neno lake. Nisikilizeni enyi watu wote, yatazameni mateso yangu. Wasichana wangu na wavulana wangu, wamechukuliwa mateka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 “Lakini Mwenyezi-Mungu amefanya sawa kwa maana nimeliasi neno lake. Nisikilizeni enyi watu wote, yatazameni mateso yangu. Wasichana wangu na wavulana wangu, wamechukuliwa mateka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 “Lakini Mwenyezi-Mungu amefanya sawa kwa maana nimeliasi neno lake. Nisikilizeni enyi watu wote, yatazameni mateso yangu. Wasichana wangu na wavulana wangu, wamechukuliwa mateka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 “Mwenyezi Mungu ni mwenye haki, hata hivyo niliasi dhidi ya amri yake. Sikilizeni, enyi mataifa yote, tazameni maumivu yangu. Wasichana wangu na wavulana wangu wameenda uhamishoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 “bwana ni mwenye haki, hata hivyo niliasi dhidi ya amri yake. Sikilizeni, enyi mataifa yote, tazameni maumivu yangu. Wavulana wangu na wasichana wangu wamekwenda uhamishoni.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.

Tazama sura Nakili




Maombolezo 1:18
38 Marejeleo ya Msalaba  

akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, BWANA asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya BWANA, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru BWANA, Mungu wako,


Na baada ya hayo yote yaliyotupata kwa sababu ya matendo yetu mabaya, na kwa sababu ya hatia yetu iliyo kuu, ikiwa wewe Mungu wetu hukutuadhibu kama tulivyostahili kwa maovu yetu, maana umetupa mabaki;


Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.


Lakini wewe u mwenye haki, katika hayo yote yaliyotupata; maana wewe umetenda yaliyo kweli, lakini sisi tumetenda yaliyo maovu;


Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu, Wakalidharau shauri lake Aliye Juu.


Ee BWANA, Wewe ndiwe mwenye haki, Na hukumu zako ni za adili.


Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa.


BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye huruma katika matendo yake yote.


Farao akatuma watu, na kuwaita Musa na Haruni, na kuwaambia, Mimi nimekosa wakati huu; BWANA ni mwenye haki, na mimi na watu wangu tu waovu.


Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?


nao wakaingia, wakaimiliki; lakini hawakuitii sauti yako, wala hawakuenda katika sheria yako; hawakutenda neno lolote katika haya uliyowaagiza wayatende; basi, kwa sababu hii umeleta juu yao mabaya haya yote;


Kama watu walindao shamba, wameuzunguka wauhusuru; kwa sababu ameniasi mimi, asema BWANA.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, wale wasioandaliwa kunywea kikombe, watakinywea, ni hakika; na wewe je! U mtu ambaye hataadhibiwa kabisa? Hukosi utaadhibiwa, naam, kunywa utakunywa.


Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia, Angalieni, mtazame Kama kuna majonzi yoyote mfano wa majonzi yangu, Niliyotendwa mimi, Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayo Siku ya hasira yake iwakayo.


Sisi tumekosa na kuasi; Wewe hukusamehe.


Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi.


tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;


Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna aibu, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa.


Siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kwa kiu.


BWANA kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya.


Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.


Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,


Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;


Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.


Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vidole vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo hivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko.


Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama uovu na kuabudu vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo