Mfalme akasema, Nina nini na ninyi, enyi wana wa Seruya? Kwa sababu yeye analaani, na kwa sababu BWANA amemwambia, Mlaani Daudi, basi, ni nani atakayesema, Mbona umetenda haya?
Maombolezo 3:38 - Swahili Revised Union Version Je! Katika kinywa chake Aliye Juu Hayatoki maovu na mema? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maafa na mema hutokea tu kwa amri yake Mungu Mkuu. Biblia Habari Njema - BHND Maafa na mema hutokea tu kwa amri yake Mungu Mkuu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maafa na mema hutokea tu kwa amri yake Mungu Mkuu. Neno: Bibilia Takatifu Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana ndiko yatokako maafa na mambo mema? Neno: Maandiko Matakatifu Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana ndiko yatokako maafa na mambo mema? BIBLIA KISWAHILI Je! Katika kinywa chake Aliye Juu Hayatoki maovu na mema? |
Mfalme akasema, Nina nini na ninyi, enyi wana wa Seruya? Kwa sababu yeye analaani, na kwa sababu BWANA amemwambia, Mlaani Daudi, basi, ni nani atakayesema, Mbona umetenda haya?
Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lolote litakalofuata baada yake.
Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.
Maana BWANA asema hivi, Kama nilivyoleta mabaya haya yote makuu juu ya watu hawa, vivyo hivyo nitaleta juu yao mema hayo yote niliyowaahidi.
Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?