Nilikuwa katika raha, naye akanivunjavunja; Naam, amenishika shingo, na kuniponda; Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.
Maombolezo 3:3 - Swahili Revised Union Version Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amenyosha mkono wake dhidi yangu mimi tu, akanichapa tena na tena mchana kutwa. Biblia Habari Njema - BHND Amenyosha mkono wake dhidi yangu mimi tu, akanichapa tena na tena mchana kutwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amenyosha mkono wake dhidi yangu mimi tu, akanichapa tena na tena mchana kutwa. Neno: Bibilia Takatifu hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa. Neno: Maandiko Matakatifu hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa. BIBLIA KISWAHILI Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. |
Nilikuwa katika raha, naye akanivunjavunja; Naam, amenishika shingo, na kuniponda; Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.
Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote;
Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.
BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu.