Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 6:4 - Swahili Revised Union Version

4 Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Naam, mishale ya Mungu Mwenye Nguvu imenichoma; nafsi yangu imekunywa sumu yake. Vitisho vya Mungu vimenikabili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Naam, mishale ya Mungu Mwenye Nguvu imenichoma; nafsi yangu imekunywa sumu yake. Vitisho vya Mungu vimenikabili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Naam, mishale ya Mungu Mwenye Nguvu imenichoma; nafsi yangu imekunywa sumu yake. Vitisho vya Mungu vimenikabili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, roho yangu inakunywa sumu yake; vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, roho yangu inakunywa sumu yake; vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.

Tazama sura Nakili




Yobu 6:4
30 Marejeleo ya Msalaba  

Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesagasaga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.


Majeshi yake husongea pamoja, na kunipandishia njia yao, Na kupiga kambi kuizunguka hema yangu.


Atanyonya sumu ya majoka; Na ulimi wa fira utamwua.


Macho yake mwenyewe na yaone uharibifu wake, Akanywe ghadhabu zake Mwenyezi.


Vitisho vimenigeukia; Huifukuza heshima yangu kama upepo; Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.


Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.


Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo; Jeraha langu haliponyeki, nijapokuwa sina makosa.


Ikiwa nimefanya dhambi, nikufanyieje, Ee mlinda wanadamu? Mbona umeniweka niwe shabaha yako, Hata nimekuwa mzigo kwa nafsi yangu?


Yeye anipondaye kwa dhoruba, Na kuyaongeza majeraha yangu pasipokuwa na sababu.


Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.


Akaipiga mishale yake akawatawanya, Naam, umeme mwingi sana, akawatapanya.


Kwa maana utawatimua utawafanya wakimbie, Kwa upote wa uta wako utazilenga nyuso zao.


Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata.


Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu.


Mishale yako ni mikali, katika mioyo ya adui za mfalme; Watu huanguka chini yako.


Naye amemtengenezea silaha za kuua, Akifanya mishale yake kuwa mipini ya moto.


Moyo huujua uchungu wa nafsi yake, Wala mgeni haishiriki furaha yake.


Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake; Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?


Kila wakati litakapopita litawachukueni. Maana litapita asubuhi baada ya asubuhi, wakati wa mchana na wakati wa usiku; na kuifahamu habari ile kutakuwa kitisho tu.


Ameupinda upinde wake kama adui, Amesimama na mkono wake wa kulia kama mtesi; Naye amewaua hao wote Waliopendeza macho; Katika hema ya binti Sayuni Amemimina ghadhabu yake kama moto.


Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote.


Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?


Basi tukiijua hofu ya Bwana, twawavuta wanadamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia.


Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.


Akawaambia, Msiniite Naomi, niiteni Mara kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo