Malaki 2:13 - Swahili Revised Union Version Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zaidi ya hayo yote, mnaifunika madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kwa machozi yenu, mkilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena tambiko mnazomtolea. Biblia Habari Njema - BHND Zaidi ya hayo yote, mnaifunika madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kwa machozi yenu, mkilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena tambiko mnazomtolea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zaidi ya hayo yote, mnaifunika madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kwa machozi yenu, mkilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena tambiko mnazomtolea. Neno: Bibilia Takatifu Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya Mwenyezi Mungu kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu. Neno: Maandiko Matakatifu Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya bwana kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu. BIBLIA KISWAHILI Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia. |
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Basi, usiwaombee watu hawa, wala usipaze sauti yako, wala kuwaombea dua watu hawa; maana sitawasikia wakati watakaponililia kwa ajili ya taabu yao.
Wafungapo, mimi sitasikia kilio chao; na watoapo sadaka za kuteketezwa na sadaka ya unga, sitazitakabali; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni.
Yafaa nini niletewe ubani kutoka Sheba, na udi kutoka nchi iliyo mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliwi, wala dhabihu zenu haziniridhii.
Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.
Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.
katika vitu hivyo sikula wakati wa kukaa matanga mimi, wala sikuviondoa nikiwa na unajisi, wala sikutoa kwa ajili ya wafu katika vitu hivyo; sauti ya BWANA, Mungu wangu, nimeisikiza, nimefanya yote, kama ulivyoniamuru.