Malaki 1:1 - Swahili Revised Union Version Ufunuo wa neno la BWANA kwa Israeli kwa mkono wa Malaki Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kauli ya Mwenyezi-Mungu iliyomjia Malaki awaambie Waisraeli. Biblia Habari Njema - BHND Kauli ya Mwenyezi-Mungu iliyomjia Malaki awaambie Waisraeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kauli ya Mwenyezi-Mungu iliyomjia Malaki awaambie Waisraeli. Neno: Bibilia Takatifu Neno la unabii: Neno la Mwenyezi Mungu kwa Israeli kupitia kwa Malaki. Neno: Maandiko Matakatifu Ujumbe: Neno la bwana kwa Israeli kupitia kwa Malaki. BIBLIA KISWAHILI Ufunuo wa neno la BWANA kwa Israeli kwa mkono wa Malaki |
Na watu hawa, au nabii au kuhani, atakapokuuliza, akisema, Mzigo wa BWANA ni nini? Ndipo utawaambia, Mzigo gani? BWANA asema, Nitawatupilia mbali.
Katika mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake nabii Hagai, kusema,
Katika mwezi wa saba, siku ya ishirini na moja ya mwezi, neno la BWANA lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,
Ufunuo wa neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.
Ufunuo wa neno la BWANA, lililosemwa juu ya nchi ya Hadraki, na Dameski itakuwa mahali pake pa kustarehe; kwa maana jicho la mwanadamu na la kabila zote za Israeli linamwelekea BWANA;
Yuda ametenda kwa hiana, na chukizo limetendeka katika Israeli, na katika Yerusalemu; maana Yuda ameunajisi utakatifu wa BWANA aupendao, naye amemwoa binti ya mungu mgeni.