Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Luka 5:11 - Swahili Revised Union Version Hata walipokwisha kuziegesha mashua zao pwani, wakaacha vyote wakamfuata. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, baada ya kuzileta zile mashua ukingoni mwa ziwa, wakaacha yote, wakamfuata. Biblia Habari Njema - BHND Basi, baada ya kuzileta zile mashua ukingoni mwa ziwa, wakaacha yote, wakamfuata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, baada ya kuzileta zile mashua ukingoni mwa ziwa, wakaacha yote, wakamfuata. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo wakasogeza mashua zao hadi ufuoni mwa bahari, wakaacha kila kitu na kumfuata. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo wakasogeza mashua zao mpaka ufuoni mwa bahari, wakaacha kila kitu na kumfuata. BIBLIA KISWAHILI Hata walipokwisha kuziegesha mashua zao pwani, wakaacha vyote wakamfuata. |
Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Nenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.