Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.
Luka 23:20 - Swahili Revised Union Version Basi Pilato alisema nao mara ya pili, kwa vile alivyotaka kumfungua Yesu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Pilato alitaka kumwachilia Yesu, hivyo akasema nao tena; Biblia Habari Njema - BHND Pilato alitaka kumwachilia Yesu, hivyo akasema nao tena; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Pilato alitaka kumwachilia Yesu, hivyo akasema nao tena; Neno: Bibilia Takatifu Pilato, akitaka kumwachia Isa, akasema nao tena. Neno: Maandiko Matakatifu Pilato, akitaka kumwachia Isa, akasema nao tena. BIBLIA KISWAHILI Basi Pilato alisema nao mara ya pili, kwa vile alivyotaka kumfungua Yesu. |
Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.
Pilato kwa kupenda kuwaridhisha watu, akawafungulia Baraba; akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, ili asulubiwe.
Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari.