Luka 2:29 - Swahili Revised Union Version Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, umruhusu mtumishi wako aende kwa amani. Biblia Habari Njema - BHND “Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, umruhusu mtumishi wako aende kwa amani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, umruhusu mtumishi wako aende kwa amani. Neno: Bibilia Takatifu “Bwana Mungu Mwenyezi, kama ulivyoahidi, sasa mruhusu mtumishi wako aende kwa amani. Neno: Maandiko Matakatifu “Bwana Mwenyezi, kama ulivyoahidi, sasa wamruhusu mtumishi wako aende zake kwa amani. BIBLIA KISWAHILI Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; |
Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai.
Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana;
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mkweli, utakawia hadi lini kuhukumu na kuilipa damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?