Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Luka 2:26 - Swahili Revised Union Version Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Biblia Habari Njema - BHND Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Neno: Bibilia Takatifu Roho wa Mungu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Al-Masihi wa Bwana. Neno: Maandiko Matakatifu Roho wa Mwenyezi Mungu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Al-Masihi wa Bwana Mwenyezi. BIBLIA KISWAHILI Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. |
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.
Nami nawaambia kweli, Wapo katika hawa wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata wauone kwanza ufalme wa Mungu.
Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).
Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake.
Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Inawezekana kuwa huyu ndiye Kristo?
habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewaambia ninyi habari zake ndiye Kristo.
Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo.
Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.