Katika vizazi vyako vyote, kila mtoto wa kiume miongoni mwenu atatahiriwa akiwa na umri wa siku nane, awe mtumishi aliyezaliwa katika nyumba yako au uliyemnunua kwa fedha zako japo hakuwa wa uzao wako.
Luka 2:21 - Swahili Revised Union Version Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. Biblia Habari Njema - BHND Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. Neno: Bibilia Takatifu Hata zilipotimia siku nane, uliokuwa wakati wa kumtahiri mtoto, akaitwa Isa, jina alilopewa na malaika kabla hajatungwa mimba. Neno: Maandiko Matakatifu Hata zilipotimia siku nane, ulikuwa ndio wakati wa kumtahiri mtoto, akaitwa Isa, jina alilokuwa amepewa na malaika kabla hajatungwa mimba. BIBLIA KISWAHILI Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. |
Katika vizazi vyako vyote, kila mtoto wa kiume miongoni mwenu atatahiriwa akiwa na umri wa siku nane, awe mtumishi aliyezaliwa katika nyumba yako au uliyemnunua kwa fedha zako japo hakuwa wa uzao wako.
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.
Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Ndipo akakubali.
tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.