Luka 19:41 - Swahili Revised Union Version Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia Biblia Habari Njema - BHND Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia Neno: Bibilia Takatifu Alipokaribia Yerusalemu na kuuona mji, aliulilia, Neno: Maandiko Matakatifu Alipokaribia Yerusalemu na kuuona mji, aliulilia, BIBLIA KISWAHILI Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, |
Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu.
Maana BWANA ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhibika kama vile katika bonde la Gibeoni; apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu; na kulitimiza tendo lake, tendo lake la ajabu.
Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa mateka.
Mimi hapa sikufanya haraka kuacha kuwa mchungaji nyuma yako; wala sikuitamani siku ya maradhi ya kuua; wewe unajua; yaliyotoka midomoni mwangu yalikuwa mbele za uso wako.
Laiti kichwa changu kingekuwa maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili nipate kulia mchana na usiku kwa ajili yao waliouawa wa binti ya watu wangu!
Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.
akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.