Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo wake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo wake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.
Luka 19:10 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.” Biblia Habari Njema - BHND Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. |
Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo wake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo wake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.
Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliotangatanga, nitawatibu waliojeruhiwa, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.
Angalieni msidharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [
Bali ilibidi kusherehekea na kushangilia kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.
Au ni mwanamke gani aliye na shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hadi aione?
Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.
Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.