Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Luka 19:1 - Swahili Revised Union Version Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. Biblia Habari Njema - BHND Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. Neno: Bibilia Takatifu Isa akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. Neno: Maandiko Matakatifu Isa akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. BIBLIA KISWAHILI Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. |
Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Wakafika Yeriko; alipokuwa akiondoka kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia.
Ikawa alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka;
Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri.
Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Nendeni mkaitazame nchi hii, hasa Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.