Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Wafalme 16:34 - Swahili Revised Union Version

34 Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Wakati wa utawala wake, Hieli kutoka Betheli, aliujenga upya mji wa Yeriko. Na sawa kabisa na neno la Mwenyezi-Mungu alilonena kwa njia ya Yoshua mwana wa Nuni, Hieli alifiwa na mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, wakati wa kuiweka misingi ya Yeriko, akafiwa pia na mwanawe mdogo Segubu, wakati wa kuyaweka malango yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Wakati wa utawala wake, Hieli kutoka Betheli, aliujenga upya mji wa Yeriko. Na sawa kabisa na neno la Mwenyezi-Mungu alilonena kwa njia ya Yoshua mwana wa Nuni, Hieli alifiwa na mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, wakati wa kuiweka misingi ya Yeriko, akafiwa pia na mwanawe mdogo Segubu, wakati wa kuyaweka malango yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Wakati wa Ahabu, Hieli ule Mbetheli, akaijenga Yeriko upya. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kama Mwenyezi Mungu alivyonena kupitia kwa Yoshua, mwana wa Nuni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Katika wakati wa Ahabu, Hieli, Mbetheli, akaijenga upya Yeriko. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kulingana na neno la bwana alilosema kupitia Yoshua mwana wa Nuni.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

34 Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.

Tazama sura Nakili

1 Wafalme 16:34
6 Marejeleo ya Msalaba  

Watu walipomwambia Daudi habari hizo, akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wameaibika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.

Watu wa Yeriko, mia tatu arubaini na watano.

Je, Baba zenu wako wapi? Je, manabii nao wanaishi milele?

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe na BWANA mtu yule atakayeinuka na kutaka kuujenga tena mji huu wa Yeriko; atakayeweka msingi wake mzaliwa wake wa kwanza na afe. Tena atakayesimamisha malango yake mtoto wake wa kiume aliye mdogo na afe.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo