Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Luka 17:13 - Swahili Revised Union Version wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakapaza sauti wakisema, “Yesu Mwalimu, tuonee huruma!” Biblia Habari Njema - BHND Wakapaza sauti wakisema, “Yesu Mwalimu, tuonee huruma!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakapaza sauti wakisema, “Yesu Mwalimu, tuonee huruma!” Neno: Bibilia Takatifu wakapaza sauti, wakasema, “Isa, Bwana, tuhurumie!” Neno: Maandiko Matakatifu wakapaza sauti, wakasema, “Isa, Bwana, tuhurumie!” BIBLIA KISWAHILI wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! |
Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi.
Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia.
Alipowaona aliwaambia, Nendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.