Abrahamu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akaharakisha kuiandaa.
Luka 15:23 - Swahili Revised Union Version mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mchinjeni ndama mnono; tule na kusherehekea! Biblia Habari Njema - BHND Mchinjeni ndama mnono; tule na kusherehekea! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mchinjeni ndama mnono; tule na kusherehekea! Neno: Bibilia Takatifu Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi. Neno: Maandiko Matakatifu Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi. BIBLIA KISWAHILI mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; |
Abrahamu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akaharakisha kuiandaa.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
Chakula cha mboga palipo na upendo; Ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.
Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.
Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;
kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.
Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya mkate wa mofa kwa unga huo;