Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.
Luka 13:13 - Swahili Revised Union Version Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Isa alipomwekea mikono yake, akasimama wima mara moja, akaanza kumtukuza Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Isa alipomwekea mikono yake, mara akasimama wima akaanza kumtukuza Mungu. BIBLIA KISWAHILI Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. |
Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.
watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.
akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yuko karibu kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.
Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.
Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi.
Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.
Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya.
Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.