Mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Eliya; akajikaza viuno, akapiga mbio akatangulia Ahabu mpaka kuiingia Yezreeli.
Luka 12:35 - Swahili Revised Union Version Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Muwe tayari mmejifunga mkanda kiunoni, na taa zenu ziwe zinawaka; Biblia Habari Njema - BHND “Muwe tayari mmejifunga mkanda kiunoni, na taa zenu ziwe zinawaka; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Muwe tayari mmejifunga mkanda kiunoni, na taa zenu ziwe zinawaka; Neno: Bibilia Takatifu “Kuweni tayari mkiwa mmevikwa kwa ajili ya huduma na taa zenu zikiwa zinawaka, Neno: Maandiko Matakatifu “Kuweni tayari mkiwa mmevikwa kwa ajili ya huduma na taa zenu zikiwa zinawaka, BIBLIA KISWAHILI Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; |
Mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Eliya; akajikaza viuno, akapiga mbio akatangulia Ahabu mpaka kuiingia Yezreeli.
Miongoni mwao hakuna achokaye wala kukwaa; Hakuna asinziaye wala kulala usingizi; Wala mshipi wa viuno vyao hautalegea. Wala ukanda wa viatu vyao hautakatika;
Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.
Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Kwa hiyo iweni tayari, na makini; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.