BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, BWANA?
Luka 12:12 - Swahili Revised Union Version kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisheni kile mnachopaswa kusema.” Biblia Habari Njema - BHND Kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisheni kile mnachopaswa kusema.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisheni kile mnachopaswa kusema.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana Roho wa Mungu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana Roho wa Mwenyezi Mungu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema.” BIBLIA KISWAHILI kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema. |
BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, BWANA?
Lakini hapo watakapowapeleka, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.
kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.
Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,
Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kulia wa Mungu.