Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Isaya 59:8 - Swahili Revised Union Version Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika mienendo yao; wamejifanyia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Njia ya amani hamwijui kamwe; njia zenu zote ni za dhuluma. Mmejifanyia njia potovu, yeyote anayepitia humo hapati amani. Biblia Habari Njema - BHND Njia ya amani hamwijui kamwe; njia zenu zote ni za dhuluma. Mmejifanyia njia potovu, yeyote anayepitia humo hapati amani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Njia ya amani hamwijui kamwe; njia zenu zote ni za dhuluma. Mmejifanyia njia potovu, yeyote anayepitia humo hapati amani. Neno: Bibilia Takatifu Hawajui njia ya amani, hakuna haki katika mapito yao. Wameyageuza kuwa njia za upotovu, hakuna apitaye njia hizo atakayeifahamu amani. Neno: Maandiko Matakatifu Hawajui njia ya amani, hakuna haki katika mapito yao. Wameyageuza kuwa njia za upotovu, hakuna apitaye njia hizo atakayeifahamu amani. BIBLIA KISWAHILI Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika mienendo yao; wamejifanyia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani. |
Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana; Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa.
Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.
Sisi sote twanguruma kama dubu; twaomboleza kama hua; twatazamia hukumu ya haki, lakini hapana; na wokovu, lakini u mbali nasi.
Kwa sababu hiyo hukumu ya haki iko mbali nasi, wala haki haitufikii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu.
Nitazameni, nitazameni. Mchana kutwa nimewanyoshea mikono yangu watu walioasi, watu waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe;
Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.