Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 59:9 - Swahili Revised Union Version

9 Kwa sababu hiyo hukumu ya haki iko mbali nasi, wala haki haitufikii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Ndio maana haki iko mbali nasi, maongozi ya uadilifu hayapo kwetu. Tunatazamia kupata mwanga kumbe ni giza tupu, twatazamia mwangaza, lakini twatembea gizani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Ndio maana haki iko mbali nasi, maongozi ya uadilifu hayapo kwetu. Tunatazamia kupata mwanga kumbe ni giza tupu, twatazamia mwangaza, lakini twatembea gizani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Ndio maana haki iko mbali nasi, maongozi ya uadilifu hayapo kwetu. Tunatazamia kupata mwanga kumbe ni giza tupu, twatazamia mwangaza, lakini twatembea gizani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Hivyo uadilifu uko mbali nasi, nayo haki haitufikii. Tunatazamia nuru, kumbe! Yote ni giza, tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza nene.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Hivyo uadilifu uko mbali nasi, nayo haki haitufikii. Tunatazamia nuru, kumbe! Yote ni giza, tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza kuu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Kwa sababu hiyo hukumu ya haki iko mbali nasi, wala haki haitufikii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu.

Tazama sura Nakili




Isaya 59:9
21 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita, Na kutia giza katika mapito yangu.


Hapo nilipotazamia mema, ndipo yakaja mabaya; Nami nilipongojea mwanga, likaja giza.


Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.


Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.


Nao watanguruma juu yao siku hiyo Kama ngurumo ya bahari; Na mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhiki Nayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake.


Sisi sote twanguruma kama dubu; twaomboleza kama hua; twatazamia hukumu ya haki, lakini hapana; na wokovu, lakini u mbali nasi.


Na hukumu imegeuka ikaenda nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia.


Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika mienendo yao; wamejifanyia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.


Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;


nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapatakuwa changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.


Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.


Je! Umemkataa Yuda kabisa? Roho yako imeichukia Sayuni? Mbona umetupiga, tusiwe na dawa ya kutuponya? Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote, tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!


Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote; tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!


Ameniongoza na kunipeleka katika giza Wala si katika nuru.


Hutangatanga njiani kama vipofu, Wametiwa unajisi kwa damu; Hata ikawa hakuna aliyeweza Kuyagusa mavazi yao.


Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana.


Maana wakazi wa Marothi wanasubiri kwa hamu kupata mema; Lakini maangamizi yameshuka toka kwa BWANA, Yamefika katika lango la Yerusalemu.


Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;


Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo