Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 59:10 - Swahili Revised Union Version

10 Twapapasapapasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walionenepa tumekuwa kama wafu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kama vipofu twapapasapapasa ukuta; tunasitasita kama watu wasio na macho. Tunajikwaa mchana kana kwamba ni usiku, miongoni mwa wenye nguvu sisi ni kama wafu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kama vipofu twapapasapapasa ukuta; tunasitasita kama watu wasio na macho. Tunajikwaa mchana kana kwamba ni usiku, miongoni mwa wenye nguvu sisi ni kama wafu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kama vipofu twapapasapapasa ukuta; tunasitasita kama watu wasio na macho. Tunajikwaa mchana kana kwamba ni usiku, miongoni mwa wenye nguvu sisi ni kama wafu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Tunapapasa ukuta kama vipofu, tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho. Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza; kati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Tunapapasa ukuta kama vipofu, tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho. Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza; katikati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Twapapasapapasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walionenepa tumekuwa kama wafu.

Tazama sura Nakili




Isaya 59:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vile vile kama usiku.


Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.


Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.


Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.


Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.


Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.


Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani.


Hutangatanga njiani kama vipofu, Wametiwa unajisi kwa damu; Hata ikawa hakuna aliyeweza Kuyagusa mavazi yao.


Nimeweka ncha ya upanga huo juu ya malango yao yote, ili mioyo yao iyeyuke, yakaongezeke makwazo yao; aha! Umefanywa kuwa kama umeme, umenolewa, ili uchinje.


Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana.


Kwa hiyo itakuwa usiku kwenu, msipate kuona maono; tena itakuwa giza kwenu, msiweze kubashiri; nalo jua litawachwea manabii, nao mchana utakuwa mweusi juu yao.


Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Nendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.


Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.


utakwenda kwa kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.


Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yuko katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo