Basi mpanda farasi mmoja akatoka awalaki, akasema, Mfalme asema hivi, Je! Ni amani? Yehu akasema, Wewe una nini na amani? Geuka unifuate. Yule mlinzi akatoa habari, akasema, Yule mjumbe amewafikia, lakini harudi tena.
Isaya 48:22 - Swahili Revised Union Version Hapana amani kwa waovu, asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu waovu sitawapa amani.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu waovu sitawapa amani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu waovu sitawapa amani.” Neno: Bibilia Takatifu “Hakuna amani kwa waovu,” asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu “Hakuna amani kwa waovu,” asema bwana. BIBLIA KISWAHILI Hapana amani kwa waovu, asema BWANA. |
Basi mpanda farasi mmoja akatoka awalaki, akasema, Mfalme asema hivi, Je! Ni amani? Yehu akasema, Wewe una nini na amani? Geuka unifuate. Yule mlinzi akatoa habari, akasema, Yule mjumbe amewafikia, lakini harudi tena.
Ndipo akapeleka mpanda farasi wa pili, naye akawafikia, akasema, Mfalme asema hivi, Je! Ni amani? Yehu akasema, Wewe una nini na amani? Geuka unifuate.
Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi makabila ya watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu.
Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka.
Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.