Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Wafalme 9:19 - Swahili Revised Union Version

19 Ndipo akapeleka mpanda farasi wa pili, naye akawafikia, akasema, Mfalme asema hivi, Je! Ni amani? Yehu akasema, Wewe una nini na amani? Geuka unifuate.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Ndipo mjumbe wa pili akatumwa, ambaye pia alimwuliza Yehu swali hilohilo. Yehu akamwambia vivyo hivyo, “Kwa nini unauliza kuhusu amani? Wewe geuka ufuatane nami!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Ndipo mjumbe wa pili akatumwa, ambaye pia alimwuliza Yehu swali hilohilo. Yehu akamwambia vivyo hivyo, “Kwa nini unauliza kuhusu amani? Wewe geuka ufuatane nami!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Ndipo mjumbe wa pili akatumwa, ambaye pia alimwuliza Yehu swali hilohilo. Yehu akamwambia vivyo hivyo, “Kwa nini unauliza kuhusu amani? Wewe geuka ufuatane nami!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Basi mfalme akamtuma mpanda farasi wa pili. Alipowafikia akasema, “Hivi ndivyo asemavyo mfalme, ‘Je, mmekuja kwa amani?’ ” Yehu akajibu, “Una nini na amani? Unga msafara nyuma yangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Basi mfalme akamtuma mpanda farasi wa pili. Wakati alipowafikia akasema, “Hivi ndivyo asemavyo mfalme, ‘Je, mmekuja kwa amani?’ ” Yehu akajibu, “Una nini na amani? Unga msafara nyuma yangu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Ndipo akapeleka mpanda farasi wa pili, naye akawafikia, akasema, Mfalme asema hivi, Je! Ni amani? Yehu akasema, Wewe una nini na amani? Geuka unifuate.

Tazama sura Nakili

2 Wafalme 9:19
5 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Yehu akatoka akawaendea watumishi wa bwana wake. Mmoja wao akamwuliza, Je! Ni amani? Huyu mwenye wazimu amekujia kwa nini? Akawaambia, Ninyi mnamjua mtu huyu na habari ya maneno yake.

Basi mlinzi alikuwa anasimama juu ya mnara wa Yezreeli, akaliona lile kundi la watu wa Yehu, alipokuwa akija, akasema, Naona kundi la watu. Yoramu akasema, Haya! Mtwae mpanda farasi mmoja, ukampeleke aende kuwalaki, na kuwauliza, Je! Ni amani?

Basi mpanda farasi mmoja akatoka awalaki, akasema, Mfalme asema hivi, Je! Ni amani? Yehu akasema, Wewe una nini na amani? Geuka unifuate. Yule mlinzi akatoa habari, akasema, Yule mjumbe amewafikia, lakini harudi tena.

Yule mlinzi akatoa habari, akasema, Amewafikia wala harudi tena; na mwendo huu ni kama mwendo wa Yehu mwana wa Nimshi; maana analiendesha gari kwa kasi.

Hapana amani kwa waovu, asema BWANA.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo