Isaya 38:12 - Swahili Revised Union Version Makao yangu yameondolewa kabisa, yamechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makao yangu yamengolewa kwangu, kama hema la mchungaji; kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu; Mungu amenikatilia mbali; kabla hata mwisho wa siku amenikomesha. Biblia Habari Njema - BHND Makao yangu yamengolewa kwangu, kama hema la mchungaji; kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu; Mungu amenikatilia mbali; kabla hata mwisho wa siku amenikomesha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makao yangu yameng'olewa kwangu, kama hema la mchungaji; kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu; Mungu amenikatilia mbali; kabla hata mwisho wa siku amenikomesha. Neno: Bibilia Takatifu Kama hema la mchunga mifugo, nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu. Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu, naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi. Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Kama hema la mchunga mifugo, nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu. Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu, naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi. Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu. BIBLIA KISWAHILI Makao yangu yameondolewa kabisa, yamechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza. |
Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda; Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!
Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.
Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama kipenu katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa.
Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.
Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twapumua kwa shida, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
Na kama mavazi utazikunjakunja, na kama mavazi zitabadilishwa; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma.
lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.