Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 38:12 - Swahili Revised Union Version

12 Makao yangu yameondolewa kabisa, yamechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Makao yangu yamengolewa kwangu, kama hema la mchungaji; kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu; Mungu amenikatilia mbali; kabla hata mwisho wa siku amenikomesha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Makao yangu yamengolewa kwangu, kama hema la mchungaji; kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu; Mungu amenikatilia mbali; kabla hata mwisho wa siku amenikomesha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Makao yangu yameng'olewa kwangu, kama hema la mchungaji; kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu; Mungu amenikatilia mbali; kabla hata mwisho wa siku amenikomesha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kama hema la mchunga mifugo, nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu. Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu, naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi. Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kama hema la mchunga mifugo, nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu. Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu, naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi. Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Makao yangu yameondolewa kabisa, yamechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.

Tazama sura Nakili

Isaya 38:12
20 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.

Roho yangu imezimia, siku zangu zimekoma, Kaburi i tayari kunipokea.

Kati ya asubuhi na jioni huvunjwa-vunjwa; Waangamia milele wala hapana atiaye moyoni.

Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda; Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!

Siku zangu ni kama kivuli cha jioni, Nami ninanyauka kama majani.

Wakuu nao waliketi wakaninena, Lakini mtumishi wako atazitafakari amri zako.

Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.

Maana mchana kutwa nimepigwa, Na kuadhibiwa kila asubuhi.

Wawafutilia wanadamu mbali kama ndoto, wao ni kama majani yameayo asubuhi.

Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama kipenu katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa.

Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.

Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.

Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twapumua kwa shida, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.

Na kama mavazi utazikunjakunja, na kama mavazi zitabadilishwa; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma.

lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo