Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
Isaya 37:3 - Swahili Revised Union Version Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nao wakamwambia Isaya, “Hezekia anasema hivi, ‘Leo ni siku ya huzuni, siku ya kukemewa, na ya dharau. Sisi tumekuwa kama mama anayetaka kujifungua mtoto, lakini hana nguvu ya kumzaa. Biblia Habari Njema - BHND Nao wakamwambia Isaya, “Hezekia anasema hivi, ‘Leo ni siku ya huzuni, siku ya kukemewa, na ya dharau. Sisi tumekuwa kama mama anayetaka kujifungua mtoto, lakini hana nguvu ya kumzaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nao wakamwambia Isaya, “Hezekia anasema hivi, ‘Leo ni siku ya huzuni, siku ya kukemewa, na ya dharau. Sisi tumekuwa kama mama anayetaka kujifungua mtoto, lakini hana nguvu ya kumzaa. Neno: Bibilia Takatifu Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa. Neno: Maandiko Matakatifu Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa. BIBLIA KISWAHILI Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa. |
Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
lakini walipomgeukia BWANA, Mungu wa Israeli, katika msiba wao, na kumtafuta, akaonekana kwao.
Msifanye mioyo yenu kuwa migumu; Kama ilivyokuwa huko Meriba Kama siku ile katika Masa jangwani.
Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.
Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.
BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.
ndipo nitamwudhi Arieli; kutakuwapo maombolezo na kilio; naye atakuwa kwangu kama Arieli.
Ee BWANA, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu kila asububi, na wokovu wetu pia wakati wa taabu.
Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.
Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa kutoka kwayo.
Uchungu wa mwanamke mwenye mimba utampata; yeye ni mwana asiye na akili; maana wakati umewadia, ambao haimpasi kukawia mahali wapenyapo watoto.
Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.
Efraimu atakuwa ukiwa siku ya adhabu; katika makabila ya Israeli nimetangaza jambo litakalotukia kweli.