Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 26:16 - Swahili Revised Union Version

16 BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Ee Mwenyezi-Mungu, walipotaabika walikutafuta, walikuomba msaada ulipowaadhibu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Ee Mwenyezi-Mungu, walipotaabika walikutafuta, walikuomba msaada ulipowaadhibu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Ee Mwenyezi-Mungu, walipotaabika walikutafuta, walikuomba msaada ulipowaadhibu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Mwenyezi Mungu, walikujia katika taabu yao, wewe ulipowarudi, waliweza kuomba kwa kunong’ona tu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 bwana, walikujia katika taabu yao, wewe ulipowarudi, waliweza kuomba kwa kunong’ona tu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.

Tazama sura Nakili




Isaya 26:16
23 Marejeleo ya Msalaba  

Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake.


Uliposema, “Nitafuteni uso wangu,” Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.


Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.


Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Nilipotaka kumkumbuka Mungu nilifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.


Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta; Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.


Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;


Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.


waliambiao gogo la mti, Wewe u baba yangu; na kuliambia jiwe, Ndiwe uliyenizaa; kwa maana wamenipa mimi visogo, wala hawakunielekezea nyuso zao; lakini wakati wa taabu watasema, Simama ukatuokoe.


Wewe ukaaye Lebanoni, Ujengaye kiota chako katika mierezi, Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana, Upatapo uchungu kama wa mwanamke azaaye.


Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.


Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa mikesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa, Mwanzo wa kila njia kuu.


Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.


Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.


Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.


Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.


Wana wa Israeli wakamwambia BWANA, “Tumefanya dhambi; tufanyie yote uyaonayo kuwa ni mema; lakini tunakusihi utuokoe siku hii ya leo”.


Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo