Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Isaya 3:13 - Swahili Revised Union Version BWANA asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu yu tayari kuanza mashtaka, anasimama kuwahukumu watu wake. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu yu tayari kuanza mashtaka, anasimama kuwahukumu watu wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu yu tayari kuanza mashtaka, anasimama kuwahukumu watu wake. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu anachukua nafasi yake mahakamani, anasimama kuhukumu watu. Neno: Maandiko Matakatifu bwana anachukua nafasi yake mahakamani, anasimama kuhukumu watu. BIBLIA KISWAHILI BWANA asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu. |
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.
BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;
Kwa maana BWANA atatoa hukumu kwa watu wote kwa moto, na kwa upanga wake, nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.
Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafati; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.
Basi sasa, sikieni asemavyo BWANA; Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako.
Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli.