Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 3:14 - Swahili Revised Union Version

14 BWANA ataingia katika kuwahukumu wazee wa watu wake na wakuu wao; Ninyi ndinyi mliokula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumba zenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mwenyezi-Mungu anawashtaki wazee na wakuu wa watu wake: “Nyinyi ndio mlioliharibu shamba la mizabibu; mali walizowanyanganywa maskini zimo nyumbani kwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mwenyezi-Mungu anawashtaki wazee na wakuu wa watu wake: “Nyinyi ndio mlioliharibu shamba la mizabibu; mali walizowanyanganywa maskini zimo nyumbani kwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mwenyezi-Mungu anawashtaki wazee na wakuu wa watu wake: “Nyinyi ndio mlioliharibu shamba la mizabibu; mali walizowanyang'anywa maskini zimo nyumbani kwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Mwenyezi Mungu anaingia katika hukumu dhidi ya wazee na viongozi wa watu wake: “Ninyi ndio mlioharibu shamba langu la mizabibu, mali iliyonyang’anywa maskini imo nyumbani mwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 bwana anaingia katika hukumu dhidi ya wazee na viongozi wa watu wake: “Ninyi ndio mlioharibu shamba langu la mizabibu, mali zilizonyang’anywa maskini zimo nyumbani mwenu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 BWANA ataingia katika kuwahukumu wazee wa watu wake na wakuu wao; Ninyi ndinyi mliokula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumba zenu.

Tazama sura Nakili




Isaya 3:14
34 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea? Na kuingia hukumuni nawe?


Mwuaji huamka asubuhi kukipambazuka, huwaua maskini na wahitaji; Tena wakati wa usiku yu kama mwizi.


Wako wamwondoao matitini kwa nguvu huyo asiye na baba, Na kutwaa rehani kwa maskini;


Kwani yeye hana haja ya kumfikiria mtu zaidi, ili aende mbele za Mungu ahukumiwe.


Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Na kumkokota akiwa wavuni mwake.


Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti BWANA.


Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.


Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.


Ole wao wawekao amri zisizo za haki, na waandishi waandikao sheria za kudhulumu;


ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake, na kuwanyang'anya maskini wa watu wangu haki yao; ili wajane wawe mateka yao, na kuwafanya yatima waliofiwa na baba zao kuwa mawindo yao!


bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.


Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.


Mguu utaukanyaga chini, Naam, miguu yao walio maskini, Na hatua zao walio wahitaji.


Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika BWANA, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli.


Basi kwa ajili ya hayo Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa sababu mwalidharau neno hili, na kutumainia jeuri na ukaidi, na kuyategemea hayo;


Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.


Tazama, ninyi mnafunga ili mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Kufunga kama huku kwa siku ya leo hakutafanya sauti zenu zisikike juu.


Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.


Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali.


na kuwadhulumu maskini na wahitaji, na kuwanyang'anya watu mali yao kwa nguvu, wala hakurudisha rehani, naye ameviinulia macho vinyago, na kufanya machukizo,


nami nitawaingiza katika jangwa la mataifa, na huko ndiko nitakakoteta nanyi uso kwa uso.


Kama nilivyoteta na baba zenu katika jangwa la Misri, ndivyo nitakavyoteta nanyi, asema Bwana MUNGU.


Tena kama ukimwuzia jirani yako chochote, au kununua chochote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe;


Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


nao hukanyaga vichwa vya maskini katika mavumbi ya nchi na kuwasukuma walioteseka kutoka kwa njia yao; na mtu na baba yake wanamwendea mwanamke mmoja, na kulitia unajisi jina langu takatifu;


Lisikieni neno hili, enyi ng'ombe wa Bashani, mnaokaa juu ya mlima wa Samaria, mnaowaonea maskini, na kuwaponda wahitaji; mnaowaambia bwana zao, Haya! Leteni, tunywe.


Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.


Nao hutamani mashamba, na kuyanyakua; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake.


Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani.


Je! Hata sasa hazina za uovu zingalimo nyumbani mwa wabaya, na kipimo kilichopunguka, ambacho ni chukizo?


Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye shamba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia ua, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.


Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo