Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Isaya 16:6 - Swahili Revised Union Version

Tumesikia habari za kiburi cha Moabu, ya kwamba ni mwenye kiburi kingi; habari za majivuno yake, na kiburi chake, na ghadhabu yake; majivuno yake si kitu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Watu wa Yuda wanasema hivi: “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu, tunajua jinsi alivyojivuna mno; tumesikia juu ya majivuno, kiburi na ufidhuli wake; lakini majivuno yake hayo ni bure.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Watu wa Yuda wanasema hivi: “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu, tunajua jinsi alivyojivuna mno; tumesikia juu ya majivuno, kiburi na ufidhuli wake; lakini majivuno yake hayo ni bure.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Watu wa Yuda wanasema hivi: “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu, tunajua jinsi alivyojivuna mno; tumesikia juu ya majivuno, kiburi na ufidhuli wake; lakini majivuno yake hayo ni bure.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: kiburi chake cha kujivuna na udanganyifu, kiburi chake na ufidhuli wake, lakini majivuno yake si kitu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: kiburi chake cha kujivuna na udanganyifu, kiburi chake na ufidhuli wake, lakini majivuno yake si kitu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Tumesikia habari za kiburi cha Moabu, ya kwamba ni mwenye kiburi kingi; habari za majivuno yake, na kiburi chake, na ghadhabu yake; majivuno yake si kitu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Isaya 16:6
17 Marejeleo ya Msalaba  

Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.

Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.

Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.

Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji machafu.

Naye atanyosha mikono yake katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake.

Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;

Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo.

Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;

Mwasemaje ninyi, Sisi tu mashujaa, watu hodari wa vita.

na Moabu atagaagaa katika matapiko yake, naye atadhihakiwa. Kwa maana Israeli, je! Hakuwa dhihaka kwako?

Na Moabu ataangamizwa, asiwe taifa tena, kwa sababu alijitukuza juu ya BWANA.

Upanga uko juu ya hao wajisifuo, nao watapumbazika; upanga uko juu ya mashujaa wake, nao watafadhaika.

Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa; Sef 2:8-11; 2 Fal 3:27

Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.