kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia moja, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
Isaya 16:3 - Swahili Revised Union Version Lete shauri; kata neno; fanya kivuli chako kuwa kama usiku kati ya mchana; wafiche waliofukuzwa; usiwachongee waliopotea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wamoabu wanawaambia watu wa Yuda, “Tupeni mwongozo, tuamulieni. Enezeni ulinzi wenu juu yetu, kama vile usiku uenezavyo kivuli chake. Tuficheni sisi wakimbizi; msitusaliti sisi tuliofukuzwa. Biblia Habari Njema - BHND Wamoabu wanawaambia watu wa Yuda, “Tupeni mwongozo, tuamulieni. Enezeni ulinzi wenu juu yetu, kama vile usiku uenezavyo kivuli chake. Tuficheni sisi wakimbizi; msitusaliti sisi tuliofukuzwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wamoabu wanawaambia watu wa Yuda, “Tupeni mwongozo, tuamulieni. Enezeni ulinzi wenu juu yetu, kama vile usiku uenezavyo kivuli chake. Tuficheni sisi wakimbizi; msitusaliti sisi tuliofukuzwa. Neno: Bibilia Takatifu “Tupeni shauri, toeni uamuzi. Wakati wa adhuhuri, fanyeni kivuli chenu kama usiku. Waficheni watoro, msisaliti wakimbizi. Neno: Maandiko Matakatifu “Tupeni shauri, toeni uamuzi. Wakati wa adhuhuri, fanyeni kivuli chenu kama usiku. Waficheni watoro, msisaliti wakimbizi. BIBLIA KISWAHILI Lete shauri; kata neno; fanya kivuli chako kuwa kama usiku kati ya mchana; wafiche waliofukuzwa; usiwachongee waliopotea. |
kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia moja, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Na kivuli wakati wa joto; Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa, Kama dhoruba ipigayo ukuta.
Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.
Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usikose kumsaidia mtu aliye jamaa yako.
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu yeyote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
BWANA asema hivi, Fanyeni hukumu na haki, mkamtoe yeye aliyetekwa katika mikono ya mdhalimu; wala msiwatende mabaya mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kuwadhulumu, wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia katika mahali hapa.
Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; uache dhambi zako kwa kutenda haki, uache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za fanaka.
BWANA wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma;
kwa maana nilikuwa na njaa, mkanipa chakula; nilikuwa na kiu, mkaninywesha; nilikuwa mgeni, mkanikaribisha;
Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Ikiwa kwa kweli mnanitia mafuta niwe mfalme juu yenu, basi njoni mkakae chini ya kivuli changu; la sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.