Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 56:8 - Swahili Revised Union Version

8 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 “Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika. Licha ya hao niliokwisha kukusanya, nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 “Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika. Licha ya hao niliokwisha kukusanya, nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 “Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika. Licha ya hao niliokwisha kukusanya, nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Bwana Mungu Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye Waisraeli waliohamishwa: “Bado nitawakusanya wengine kwao zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 bwana Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye Waisraeli waliohamishwa: “Bado nitawakusanya wengine kwao zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.

Tazama sura Nakili




Isaya 56:8
25 Marejeleo ya Msalaba  

Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.


Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.


BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu, Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.


nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.


Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka magharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu.


Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwainulia makabila ya watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.


naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuyainua makabila ya Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.


Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakurudisha.


Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye.


Lisikieni neno la BWANA, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.


Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo wake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo wake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.


Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajichagulia kiongozi mmoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.


Katika siku ile, asema BWANA, nitamkusanya yeye achechemeaye, nami nitamrudisha yeye aliyefukuzwa, na yeye niliyemtesa.


Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.


Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.


Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki?


Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo