Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 21:12 - Swahili Revised Union Version

12 Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu yeyote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 enyi jamaa ya Daudi! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tekelezeni haki tangu asubuhi, na kuwakomboa mikononi mwa wadhalimu wote walionyanganywa mali zao. La sivyo, hasira yangu itachomoza kama moto, itawaka na wala hakuna atakayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yenu maovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 enyi jamaa ya Daudi! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tekelezeni haki tangu asubuhi, na kuwakomboa mikononi mwa wadhalimu wote walionyanganywa mali zao. La sivyo, hasira yangu itachomoza kama moto, itawaka na wala hakuna atakayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yenu maovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 enyi jamaa ya Daudi! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tekelezeni haki tangu asubuhi, na kuwakomboa mikononi mwa wadhalimu wote walionyang'anywa mali zao. La sivyo, hasira yangu itachomoza kama moto, itawaka na wala hakuna atakayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yenu maovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi, mwokoeni mikononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara, la sivyo ghadhabu yangu italipuka na kuwaka kama moto kwa sababu ya uovu mlioufanya: itawaka na hakuna wa kuizima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo bwana asemalo: “ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi, mwokoeni mikononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara, la sivyo ghadhabu yangu italipuka na kuwaka kama moto kwa sababu ya uovu mlioufanya: itawaka na hakuna wa kuizima.

Tazama sura Nakili




Yeremia 21:12
46 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi akatawala juu ya Israeli wote; naye Daudi akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.


Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake.


Kila asubuhi nitawaangamiza Waovu wote nchini. Nikiwatenga wote watendao uovu Na mji wa BWANA.


Asubuhi yake Musa akaketi ili awapishie hukumu watu; na hao watu wakasimama kumzunguka Musa tangu asubuhi hata jioni.


jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.


Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima.


Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia?


Kisha watu wa nyumba ya Daudi wakaambiwa kwamba Shamu wamefanya mapatano na Efraimu. Na moyo wake ukataharuki, na moyo wa watu wake, kama miti ya mwituni itikiswavyo na upepo.


Nawe, naam, wewe nafsi yako, utaachana na urithi wako niliokupa; nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana umewasha moto katika hasira yangu, utakaowaka milele.


Na mimi mwenyewe nitapigana nanyi, kwa mkono ulionyoshwa na kwa mkono hodari, naam, kwa hasira, na kwa ukali, na kwa ghadhabu nyingi.


Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni kimbunga cha tufani; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani.


Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama; angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema BWANA.


Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.


Labda wataomba dua zao mbele za BWANA, na kurudi, kila mtu akiiacha njia yake mbaya; kwa maana hasira na ghadhabu ni kuu sana, alizotamka BWANA juu ya watu hawa.


Jitahirini kwa BWANA, mkayaondoe magovi ya mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.


Hata BWANA asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.


Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika kinywa chako kuwa moto, na watu hawa kuwa kuni, nao moto utawala.


Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.


Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.


Maana kama mkitengeneza kabisa njia zenu na matendo yenu; kama mkihukumu hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake;


BWANA ameitimiza ghadhabu yake, Ameimimina hasira yake kali; Naye amewasha moto katika Sayuni Ulioiteketeza misingi yake.


Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.


ndipo nami nitawaendea kinyume katika ghadhabu yangu; nami nitawaadhibu mara saba kwa dhambi zenu.


Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.


Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.


BWANA kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya.


Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.


kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.


Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo