Lakini BWANA akawahurumia, akawasikitikia, na kuwaangalia, kwa ajili ya agano lake na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, wala hakutaka kuwaangamiza, wala hakuwatupa usoni pake bado.
Hosea 7:15 - Swahili Revised Union Version Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi ndimi niliyeiimarisha mikono yao, lakini wanafikiria maovu dhidi yangu. Biblia Habari Njema - BHND Mimi ndimi niliyeiimarisha mikono yao, lakini wanafikiria maovu dhidi yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi ndimi niliyeiimarisha mikono yao, lakini wanafikiria maovu dhidi yangu. Neno: Bibilia Takatifu Niliwafundisha na kuwatia nguvu, lakini wanapanga mabaya dhidi yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Niliwafundisha na kuwatia nguvu, lakini wanapanga mabaya dhidi yangu. BIBLIA KISWAHILI Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu. |
Lakini BWANA akawahurumia, akawasikitikia, na kuwaangalia, kwa ajili ya agano lake na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, wala hakutaka kuwaangamiza, wala hakuwatupa usoni pake bado.
(BWANA akawapa Israeli mwokozi, nao wakatoka mikononi mwa Washami; wana wa Israeli wakakaa hemani mwao kama zamani za kwanza.
Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi.
Hadi lini mtamshambulia mtu, Mpate kumwua ninyi nyote pamoja? Kama ukuta unaoinama, Kama ua ulio tayari kuanguka,
Haya ndiyo maangamizo yako, Ee Israeli, kwa kuwa wewe u kinyume changu mimi, kinyume cha msaada wako.
nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau maonyo ya Bwana, Wala usife moyo ukiadhibiwa naye;