Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nahumu 1:9 - Swahili Revised Union Version

9 Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu? Yeye atawakomesha na kuwaangamiza, wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu? Yeye atawakomesha na kuwaangamiza, wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu? Yeye atawakomesha na kuwaangamiza, wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Kila njama wanayopanga dhidi ya Mwenyezi Mungu yeye atalikomesha; taabu haitatokea mara ya pili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya bwana yeye atalikomesha; taabu haitatokea mara ya pili.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

Tazama sura Nakili




Nahumu 1:9
17 Marejeleo ya Msalaba  

Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao tumboni, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri.


Wakipanga kukutenda mabaya, Kwa miango ya hila, hawatafanikiwa.


BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huitangua mipango ya watu.


Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.


Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.


nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka. Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.


na watu wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeufuta upanga wangu alani mwake; hautarudi tena.


Bwana MUNGU asema hivi; Ni jambo baya, jambo baya la namna ya peke yake; angalia, linakuja.


Ingawa nimewafundisha na kuwatia nguvu mikono yao, hata hivyo hukusudia udhalimu juu yangu.


Ametoka mmoja kwako, akusudiaye mabaya juu ya BWANA, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.


tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;


Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hadi chini kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili.


Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli kuhusu nyumba yake, tangu mwanzo hadi mwisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo