Hosea 5:12 - Swahili Revised Union Version Kwa sababu hiyo mimi nimekuwa kama nondo kwa Efraimu, nimekuwa kama ubovu kwa nyumba ya Yuda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu, kama donda baya kwa watu wa Yuda. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu, kama donda baya kwa watu wa Yuda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu, kama donda baya kwa watu wa Yuda. Neno: Bibilia Takatifu Mimi ni kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa watu wa Yuda. Neno: Maandiko Matakatifu Mimi ni kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa watu wa Yuda. BIBLIA KISWAHILI Kwa sababu hiyo mimi nimekuwa kama nondo kwa Efraimu, nimekuwa kama ubovu kwa nyumba ya Yuda. |
Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili.
Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mwenye hatia? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala.
Maana nondo atawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote.
Lakini siku ya pili kulipopambazuka, Mungu akatayarisha buu, nalo likautafuna ule mtango, ukakatika.