Hosea 13:7 - Swahili Revised Union Version Basi nimekuwa kama simba kwao; kama chui nitavizia njiani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, nitakuwa kama simba kwenu nyote; nitawavizieni kama chui njiani. Biblia Habari Njema - BHND Basi, nitakuwa kama simba kwenu nyote; nitawavizieni kama chui njiani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, nitakuwa kama simba kwenu nyote; nitawavizieni kama chui njiani. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba, kama chui nitawavizia kando ya njia. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba, kama chui nitawavizia kando ya njia. BIBLIA KISWAHILI Basi nimekuwa kama simba kwao; kama chui nitavizia njiani; |
BWANA atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu.
Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali.
Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.
Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa.
Naye alisema, BWANA atanguruma toka Sayuni, Atatoa sauti yake toka Yerusalemu; Na malisho ya wachungaji yatakauka, Na kilele cha Karmeli kitanyauka.
Je! Simba atanguruma mwituni, asipokuwa na mawindo? Mwanasimba atalia pangoni mwake, ikiwa hakupata kitu?
Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?
Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, lile joka likampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.