Katika miungu ya nchi hizi zote, ni miungu gani iliyookoa nchi yao na mkono wangu, hata BWANA auokoe Yerusalemu na mkono wangu?
Hosea 13:4 - Swahili Revised Union Version Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu nchi ya Misri; wala hutamjua mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna mwokozi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu asema: “Lakini mimi, Mwenyezi-Mungu, ni Mungu wenu, ambaye niliwatoa nchini Misri; hamna mungu mwingine ila mimi, wala hakuna awezaye kuwaokoeni. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu asema: “Lakini mimi, Mwenyezi-Mungu, ni Mungu wenu, ambaye niliwatoa nchini Misri; hamna mungu mwingine ila mimi, wala hakuna awezaye kuwaokoeni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu asema: “Lakini mimi, Mwenyezi-Mungu, ni Mungu wenu, ambaye niliwatoa nchini Misri; hamna mungu mwingine ila mimi, wala hakuna awezaye kuwaokoeni. Neno: Bibilia Takatifu “Bali mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, niliyewaleta ninyi toka Misri. Msimkubali Mungu mwingine ila mimi, hakuna Mwokozi isipokuwa mimi. Neno: Maandiko Matakatifu “Bali mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu, niliyewaleta ninyi toka Misri. Msimkubali Mungu mwingine ila mimi, hakuna Mwokozi isipokuwa mimi. BIBLIA KISWAHILI Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu nchi ya Misri; wala hutamjua mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna mwokozi. |
Katika miungu ya nchi hizi zote, ni miungu gani iliyookoa nchi yao na mkono wangu, hata BWANA auokoe Yerusalemu na mkono wangu?
Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.
Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.
Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za sikukuu teule.
Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.