Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 12:9 - Swahili Revised Union Version

9 Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za sikukuu teule.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri! Mimi nitakukalisha tena katika mahema, kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu, wakati wa sikukuu ya vibanda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri! Mimi nitakukalisha tena katika mahema, kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu, wakati wa sikukuu ya vibanda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mwenyezi-Mungu asema, “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; mimi ndimi niliyekutoa nchini Misri! Mimi nitakukalisha tena katika mahema, kama ufanyavyo sasa kwa siku chache tu, wakati wa sikukuu ya vibanda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, niliyewaleta kutoka Misri; nitawafanya mkae tena kwenye mahema, kama vile katika siku za sikukuu zenu zilizoamriwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu niliyewaleta kutoka Misri; nitawafanya mkae tena kwenye mahema, kama vile katika siku za sikukuu zenu zilizoamriwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za sikukuu teule.

Tazama sura Nakili




Hosea 12:9
22 Marejeleo ya Msalaba  

Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani.


mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.


Wakaishika sikukuu ya vibanda, kama ilivyoandikwa, wakatoa sadaka za kuteketezwa za kila siku kwa hesabu yake, kama ilivyoagizwa, kama ilivyopasa kila siku;


Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumlipa Mungu fidia kwa ajili ya maisha yake,


Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.


Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.


Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao.


wala msijenge nyumba, wala msipande mbegu, wala msipande mizabibu, wala msiwe nayo; bali siku zenu zote mtakaa katika hema; mpate kuishi siku nyingi katika nchi ambayo mtakaa ndani yake kama wageni.


Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali.


Israeli alipokuwa mtoto, nilikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri.


Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu nchi ya Misri; wala hutamjua mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna mwokozi.


Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.


Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.


Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawafanya mwende sawasawa.


Kwa maana nilikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami niliwatuma Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako.


ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.


Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Na sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya vibanda, ilikuwa karibu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo