Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yona 2:10 - Swahili Revised Union Version

10 BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona kwenye nchi kavu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona kwenye nchi kavu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona kwenye nchi kavu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Basi Mwenyezi Mungu akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Basi bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.

Tazama sura Nakili




Yona 2:10
18 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.


Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili ya kuonesha majira, siku na miaka;


Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.


Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.


Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.


Alisema, kukaja makundi ya mainzi, Na chawa katika nchi yao yote.


Alisema, kukaja nzige, Na tunutu wasiohesabika;


Wapole watakula na kushiba, Wamtafutao BWANA watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele.


Maana Yeye alisema, na ikawa; Na Yeye aliamuru, ikaumbika.


BWANA yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.


Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi.


Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.


Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu nchi ya Misri; wala hutamjua mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna mwokozi.


Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.


BWANA akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku.


Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, kusema,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo