Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.
Hosea 12:13 - Swahili Revised Union Version Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri, Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa nabii Mwenyezi-Mungu aliwatoa Waisraeli nchini Misri, na kwa nabii Mungu aliwahifadhi. Biblia Habari Njema - BHND Kwa nabii Mwenyezi-Mungu aliwatoa Waisraeli nchini Misri, na kwa nabii Mungu aliwahifadhi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa nabii Mwenyezi-Mungu aliwatoa Waisraeli nchini Misri. na kwa nabii Mungu aliwahifadhi. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu alimtumia nabii kumpandisha Israeli kutoka Misri, kupitia kwa nabii alimtunza. Neno: Maandiko Matakatifu bwana alimtumia nabii kumpandisha Israeli kutoka Misri, kwa njia ya nabii alimtunza. BIBLIA KISWAHILI Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri, Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa. |
Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.
Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda.
Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.
Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao;
Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.
Kwa maana nilikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami niliwatuma Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako.
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumteta mtumishi wangu, huyo Musa?
Nawe ujibu, ukaseme mbele za BWANA, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi.
Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa.