Hesabu 26:11 - Swahili Revised Union Version Hata hivyo, hao wana wa Kora hawakufa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Pamoja na hayo wana wa Kora hawakufa.) Biblia Habari Njema - BHND Pamoja na hayo wana wa Kora hawakufa.) Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Pamoja na hayo wana wa Kora hawakufa.) Neno: Bibilia Takatifu Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa. Neno: Maandiko Matakatifu Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa. BIBLIA KISWAHILI Hata hivyo, hao wana wa Kora hawakufa. |
Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa ukoo wa babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ulinzi wa malango ya maskani; na kama vile baba zao walivyokuwa wamesimamia kambi ya BWANA, wakiyalinda maingilio;
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.
Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.
Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo.
nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.
Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wakiwa hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.
kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi BWANA ataonesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake.
Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini;
na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote;
Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.